Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetenga zaidi ya shilingi bilioni 900 kwaajili ya uboreshaji wa Sekta ya Kilimo na Miundombinu ya umwagiliaji, Ubora wa mbegu, upatikanaji wa mbolea, upimaji wa Afya ya udongo na kuongeza Matrekta kwaajili ya kuongeza tija katika Kilimo.
Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Mustaaf Mhe. Mizengo Pinda Agost 1, 2023 alipokua akifungua Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu Kama nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Waziri Mkuu Mustaafu amesema kuwa Fedha hizo zitawasaidia Wakulima kulima kilimo chenye tija na kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la Pato la Taifa.
Aidha, Mhe. Pinda pia amezitaka Taasisi za fedha nchini kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa mikopo kwa makundi ya Vijana na Wanawake ili kukuza Sekta ya Kilimo nchini.
Kwa upande mwingine Mhe. Pinda amesikitishwa na hali ya udumavu wa watoto chini ya umri wa miaka 5 ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na ukosefu wa lishe bora kwa Mama pindi anapokua katika hali ya ujauzito na kuongeza kuwa Mkoa wa Morogoro una tatizo la udumavu kwa 30% ambapo hapo awali ilikua 35%
Maonesho haya yanayoendelea Mkoani Morogoro kuanzia tarehe 1-8/8/2023: yanajumuisha Mikoa 4 ya Dar es salaam, Pwani, Tanga na Mwenyeji Morogoro, Maonesho haya pia yanashirikisha Taasisi mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ambapo Malinyi inashiriki kutoa Elimu kuhusu masuala mbalimbali ya Kilimo.
Malinyi pia inashiriki katika Maonesho haya kwa kuonesha Vipando vya makundi takribani 7 ya mazao ambayo ni mazao ya miti na matunda, mazao ya ndizi mbichi, mazao ya mafuta, mazao ya nafaka, mazao ya jamii ya mikunde, mazao ya mizizi, mazao ya mbogamboga pamoja na teknolojia rahisi ya kuandaa kamba ya kupandia mazao, na teknolojia ya kuhifadhia nafaka hasa mahindi.
"VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.