Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi imepokea zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule za msingi ikihusisha vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na nyumba ya Mwalimu, Katika ujenzi huo shule mbili mpya za msingi zitajengwa ambazo ni Shule ya msingi Mwembeni na Shule ya msingi Njiwa.
Akisoma muongozo wa utekelezaji wa miradi ya boost katika kikao kilichofanyika tarehe 12/6/2023 na kumuhusisha Mkurugenzi, Waalimu Wakuu, Wenyeviti wa kamati za ujenzi, Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri, Afisa manunuzi, Mkaguzi wa ndani na Maafisa elimu idara ya Elimu msingi, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe.Sebastian Waryuba amesema fedha zote ziizotolewa na Mhe.Raisi Samia Suluhu Hassan zitumike kujenga miundombinu yote iliyokusudiwa na kuzingatia ubora ili miradi hii iwe benki ya utekelezaji wa miradi ijayo.
Mhe.Mkuu wa Wilaya ametoa angalizo juu ya bei elekezi za vifaa vya ujenzi na umuhimu wa kujiridhisha na bei kabla ya kufanya manunuzi, na kukemea ununuzi wa vifaa vingi kwa mra moja bila ya kuzingatia mahitaji sahihi kuwa ni ubadhirifu wa fedha na husababisha hasara na ujenzi wa vitu vingine visivyohitajika.
Akitolea ufafanuzi juu ya uwazi na ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya boost, Mkuu wa Takukuru Wilaya Bi Sikujua Kimweri amesema Wakuu wa shule waandae vibao vinavyotoa taarifa muhimu za utekelezaji wa mradi, Wenyeviti na Watendaji wa vijiji waitishe mikutano na wawaambie wananchi kuhusu fedha zilizopokelewa na miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika eneo husika.
Aidha, Bi Sikujua Kimweri akaongeza kuwa miradi hii inatakiwa kukamilika ndani ya muda uliokusudiwa ili kuepuka kuwa na miradi mingi ambayo haijakamilika.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.