Imeelezwa kuwa Shule mpya ya Sekondari Kiswago kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari( SEQUIP) inatarajiwa kujengwa katika Kijiji Cha Kiswago, Kata ya Sofi, Tarafa ya Mtimbira.
Taarifa hiyo imetolewa Julai 18, 2023 na Afisa Elimu ya Watu Wazima Sekondari Ndugu Filoteus Nombo kwa niaba ya Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Sekondari alipokua akiutambulisha mradi wa ujenzi wa shule hiyo mpya katika mkutano uliohudhuriwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Malinyi Bi Rehema Rajabu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi pamoja na Viongozi na Wanakijiji wa Kata ya Sofi.
Ndugu Nombo amefafanua kuwa Mradi wa kuboresha Elimu Sekondari umetoa shilingi milioni 528, 998, 425 kwaajili ya ujenzi huo utakaojumuisha Vyumba vya Madarasa 8, Ofisi ndogo 2 za Waalimu, Matundu 4 ya vyoo kwa Wasichana, Matundu 4 ya vyoo kwa Wavulana, Maabara, Kichomea taka, Tanki la Maji la aridhini, Maktaba, Jengo la Utawala na Chumba cha Tehama
Ujenzi huo unatarajiwa kufanyika katika eneo lenye ukubwa wa ekari 33.5 lililotolewa na Serikali ya Kijiji cha Kiswago na pindi Mradi huo utakapokamilika utapunguza adha ya Wanafunzi kutembea umbali mrefu wa kilometa 34 hasa kwa Wanafunzi wanaotoka maeneo ya Salamiti, Mnazimmoja na Kiswago kwenda Shule ya Sekondari Sofi .
Akizungumza kwa niaba ya Wanakijiji wa Kata ya Sofi, Mhe.Diwani Lucas John Mgomahenga ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za ujenzi wa shule hiyo mpya katika Kijiji Cha Kiswago na kuongeza kuwa Wanakiji wa Kata ya Sofi wanaahidi ushirikiano wa hali juu kuanzia mwanzo wa Mradi huo mpaka pale utakapokamilika.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.