Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba ambaye pia alikua Mgeni rasmi wa kilele Cha maadhimisho ya sikukuu ya Nanenane Kanda ya Mashariki ameagiza kuwa teknolojia za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi zilizooneshwa katika maonesho ya Nanenane ziwafikie Wakulima katika maeneo yao ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji.
Mhe. Kindamba ameyasema hayo Agost 8, 2023 wakati wa kilele Cha maadhimisho ya ya sikukuu ya Nanenane Kanda ya Mashariki yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Manispaa ya Morogoro.
"Kutokana na maonesho haya ninaamini kutakua na Kilimo chenye tija kwa kujifunza teknolojia na mbinu za kisasa zinazoendana na mabadiliko ya tabia nchi kwani kwa kuongeza uzalishaji kupitia teknolojia mpya zilizotolewa katika maadhimisho haya itakua rahisi kupata masoko ya mazao hayo" amesema Mhe. Kindamba.
Aidha, Mhe. Kindamba amesema kuwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wakiwa na uzalishaji wenye tija itapelekea kukidhi mahitaji ya nchi na kupanua wigo wa biashara ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo, Mhe. Kindamba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku katika sekta ya Kilimo na kupunguza bei za viwatilifu na mbolea hali ambayo itawasaidia Wakulima wenye hali ya chini kupata pembejeo hitajika na kupekeleka kupata mazao ya kutosha
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.