Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri yalilengakuwajengea uwezo Maafisa wanaohusika na kufanya malipo katika Wilaya ya Malinyi juu ya namna sahihi ya kukata kodi ya zuio na kulipa benki ili Serikali iweze kupata mapato yake yatakayowezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya Elimu, Afya, Maji, miundombinu ya barabara n.k.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa Uhusiano Mkuu kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) Makao Makuu Idara ya elimu kwa mlipa kodi Ndugu Hadson Kamoga amesema kwamba msisitizo mkubwa wa Serikali ya awamu ya sita ni kuleta maendeleo kwa Wananchi na Wananchi wenyewe ni mashuhuda namna gani Serikali inavyoleta miradi mingi maana yake kodi inakusanywa kwani kodi isipokusanywa miradi ya maendeleo haiwezi kupatikana.
Afisa huyo amefafanua kuwa kodi ya zuio hukatwa kwa muhusika anayetoa huduma au bidhaa kabla muhusika huyo hajalipwa hivyo jukumu la maafisa hao ni kuhakikisha kila mtoa huduma au bidhaa anakatwa kodi ya zuio kwa mujibu wa sheria.
Ndugu Hadson Kamoga amesema kuwa matarajio ya Serikali kwa Maafisa hao mara baada ya kupata mafunzo hayo ni kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa na kwa kufuata kanuni taratibu na sheria ili Serikali iweze kupata mapato yake.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.