Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Pius Mwelase katika Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kwaajili ya kujadili taarifa za utekelezaji robo ya kwanza Julai-Septemba kilichofanyika 31 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Aidha, Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa katika shughuli za kimaendeleo Halmashauri imejipanga kufanya vizuri zaidi katika kuhakikisha miradi yote ya kimkakati inakwenda kukamilika kwa kutumia bajeti ya mapato ya ndani.
Pamoja na masuala mengine, Mhe. Mwelase ametoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi kuitisha kikao cha Menejimenti mapema iwezekanavyo ili kujadili mapendekezo ya barua ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Sebastiani Waryuba ambayo ameiandika hivi karibuni juu ya malalmiko kutoka kwa Wananchi kuhusu kupanda kwa tozo za ushuru wa mazao (mchele na pumba)wakati akifanya ziara za kusikiliza na kujibu kero za Wananchi katika Vijiji vya Wilaya ya Malinyi.
"Tumepokea ushauri kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, Tumepokea ushauri kutoka kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na tunaahidi kuufanyia kazi kwa haraka kwakua Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Serikali Inayowasikiliza Wananchi wake" amesema Mwenyekiti huyo wa Halmashauri
Mapema, akitoa neno la Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Bi Rehema Rajabu ameishauri Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri pamoja na matumizi yake unazingatia kanuni taratibu na sheria zilizopo katika kukusanya na kutumia fedha hizo za mapato ya ndani kwa kuzingatia 40% katika utekelezaji wa miradi, 10% kwa makundi ya Vijana , Wanawake na Watu wenye ulemavu.
Hata hivyo,Muwakilishi huyo wa Mkuu wa Wilaya alisisitiza juu ya uimarishaji wa mazao ya kimkakati kama vile ufuta, mbaazi na michikichi ili kuhakikisha kuwa uchumi wa Halmashauri unazidi kuimarika na kuongeza kuwa mamlaka zinazohsika na kusikiliza na kutatua kero za Wananchi zinasimamia suala la kero za Wananchi katika ngazi za awali kabla ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.