Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bwana Kebwe Steven Kebwe amefanya ziara wilayani Malinyi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya na Kituo cha afya Ngoheranga ambapo ujenzi huo wa kituo cha Ngoheranga unafikia hatua za mwisho . Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ambapo ujenzi huo upo nyuma sana,mkuu huyo wa mkoa ameagiza ujenzi huo ufanyike usiku na mchana ili kuharakisha umalizikaji wake,pia ametoa muda wa mwezi mmoja ujenzi wa majengo hayo uwe umekamlika.
Akiongea na viongozi wa wilaya na wakuu wa idara katika ziara hiyo ambayo imefanyika tarehe 24 april 2019, mkuu huyo amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri kusimamia ipasavyo katika kuongeza kasi ya ufyatuaji matofali ya ujenzi wa Hospital ya wilaya kutoka matofali elfu moja mpaka elfu mbili kwa siku,pia ameagiza kuongeza idadai ya mafundi wasaidizi ili kazi iweze kwenda haraka.
Katika ziara hiyo mkuu huyo alipokea taarifa ya CHF Wilayani na kuagiza uongozi wa Hospital ya Mission ya Lugala ambayo ilikuwa haipokei na kuhudumia wagonjwa wanaotumia Kadi za CHF kwa matibabu,waandae utaratibu ili kuweza kuwapokea wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ya Jamii(CHF).Vile vile ameagiza uongozi wa wilaya pamoja na mratibu wa CHF kuwahamasisha wananchi ili waweze kujiunga na CHF kwa wingi.
Akihitimisha ,Mh kebwe ameshauri Halmashauri kuweka mkakati wa kuanzisha mradi wa kilimo ambao utaweza kusaidia kupata mapato ya ndani .
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.