Nyumba ya Walimu Two in one inatarajiwa kujengwa katika Shule ya Sekondari Ndewele Kata ya Malinyi Wilayani Malinyi kwa gharama ya shilingi Milioni 95,000,000.
Akiutambulisha mradi wa ujenzi wa nyumba hiyo Agost 31, 2023 kwa Wananchi wa Kitongoji Cha Ndewele Kata ya Malinyi Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Wilaya ya Malinyi Bi Pendo Masalu amesema kuwa Mradi huu utakapokamilika utapunguza Adha ya Walimu Wanaoishi katika Kijiji cha Misegese ambao wanatembea umbali wa zaidi ya km 26 kwenda Shuleni na kurudi.
Aidha Mkuu huyo wa Divisheni ya Elimu Sekondari Wilaya ameishukuru Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za ujenzi wa Shule hiyo,na ametoa rai kwa Wananchi wa Kata ya Malinyi kumuunga mkono Mhe. Rais katika Juhudi za kuboresha Elimu na miundombinu kwa kujitolea nguvu kazi mpaka ujenzi huo utakapokamilika
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.