Moja ya matendo yanayohatarisha ustawi wa sekta ya Uvuvi ni tendo la uvuvi haramu. Katika picha hapo juu ni makokoro yaliyokuwa yakitumiwa na wavuvi katika mwambao wa mto Kilombero kwa upande wa wilaya ya Malinyi. Afisa wa uvuvi wa wilaya ya Malinyi Bw. Ogare alieleza kwamba uvuvi haramu katika mito iliyopo wilaya ya Malinyi ni tishio kwa ustawi wa sekta ya uvuvi katika wilaya hii. Akiongea kwa msisitizo Bw. Ogare alisema kuwa kwa sasa idara yake imejipanga kufanya doria za mara kwa mara katika maeneno yote yenye mito na litakuwa zoezi endelevu. Lengo kubwa la doria hizo ni kuwezesha samaki kuzaliana na kufanya samaki wapatikane kwa wingi katika wilaya ya Malinyi kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita. Kwa sasa samaki ni hadimu sana wilayani Malinyi kutokana na kukithiri kwa matukio ya uvuvi haramu. Aidha walitaka wavuvi wote kufuata taratibu za kisheria za uvuvi ili kuwa na uvuvi wenye tija.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.