Mkuu wa mkoa wa Morogoro amezindua mfuko wa afya ya jamii(CHF) kwa mwaka 2018, uzinduzi huo umefanyika tarehe 8/9/2018 katika kijiji cha Mtimbira Wilayani Malinyi,akiongea na wananchi katika uzinduzi huo mkuu huyo amewahimiza wananchi kujiunga na CHF ili kupata matibabu bila shida wakati wanapougua,ili kuepuka usumbufu wa kukosa matibabu pale wanapokuwa hawana fedha za matibabu .
Vilevile amesisitiza fedha za CHF zielekezwe katika huduma za afya tu,50% iwe kwa ajili ya dawa na asilimia iliyobaki itumike kwa kununua vifaa vingine vya tiba. Pia amewaagiza uongozi mzima wa wilaya kufanya kampeni ya kwa kila kijiji ili kuwahimizi wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya jamii ambao umepanda kutoka elfu kumi ya awali na sasa ni elfu thelathini tu .
Katika uzinduzi huo mkuu huyo wa mkoa amewakabidhi kadi zao wananchi wawili ambao wamekuwa wa mwanzo kujiunga na CHF ya elfu thelathini na pia ametoa vyeti vya pongezi kwa waandikishaji watatu ambao na vijiji ambavyo vimeandikisha wanachama wengi kwa awamu iliyopita.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.