Wasichana na Wavulana rika balehe Wilayani Malinyi wametakiwa kujikubali, kushinda vishawishi na kuwa bora ili waweze kufurahia
masomo yao na kufikaa malengo yao.
Hayo yamesemwa na muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi Rehema Rajabu katika kampeni ya mabadiliko ya tabia katika kujikinga dhidi ya maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wanafunzi wa Sekondari(vijana rika balehe) iliyofanyika katika viwanja vya shule msingi Nawigo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya VVU, mimba za utotoni na kutoa huduma rafiki za Afya.
Bi Rehema Rajabu amesema kuwa kampeni hiyo imelenga kundi la Vijana rika balehe miaka 15-24 (Wasichana, na Wavulana) kwa sababu Vijana katika umri huo hawajui hali zao za maambukizi ambapo kwa mujibu wa takwimu za mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi ni 70.2% tu ya Vijana miaka 15-24 wanaokadiriwa kuishi na VVU
Aidha, Muwakilishi huyo wa Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa takwimu za viashiria na maambukizi ya Ukimwi nchini zinaonyesha kuwa 40% ya hali ya maambukizi mapya ya VVU ni Vijana wenye umri wa miaka 15-24 ambapo kati ya watu 10 wenye maambuki wanne( 4)kati yao ni Vijana umri wa rika balehe.
Kutokana na hali hiyo, Bi Rehema Rajabu amesema kuwa Kampeni hiyo itawajengea Vijana uelewa sahihi kuhusu VVU na Ukimwi, masuala ya afya ya uzazi jambo ambalo litawawezesha Vijana kujiepusha na vishawishi, mimba za utotoni na magonjwa ya ngono.
Awali ya hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi Rehema Saidi Bwasi aliishukuru Wizara ya Afya pamoja Wadau walioshiriki kufanikisha Kampeni hiyo Wilayani Malinyi kwa kuwapa elimu Vijana rika balehe kwani hilo ndilo kundi linalokumbana na changamoto mbalimbali zinazopelekea kutofikia malengo yao.
Kufuatia hali hiyo, Vijana wametakiwa kujitambua, kuchukua hatua kwaajili ya kesho yao na kushinda vishawishi katika umri mdogo, Wazazi na Walimu watimize wajibu wao na wazungumze na Vijana ili kuwaongoza waweze kufurahia masomo yao na kufikia malengo yao.
JIKUBALI, SHINDA VISHAWISHI, KUWA BORA
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.