Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe Sebastian Waryuba ametoa tamko hilo Agosti 17, 2023 katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Biro Wilayani Malinyi ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika kutembelea miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi Wilayani Malinyi.
Mhe. Waryuba amesema kuwa mtindo wa kujivunia kuwa na idadi kubwa ya Mifugo umepitwa na wakati na amewataka Wafugaji katika Kata ya Biro kuhakikisha kuwa wanamiliki Mifugo inayotosheleza mahitaji yao na inayoendana na maeneo yao.
Mhe. Waryuba pia ameagiza kuwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Mifugo yasitumike kwaajili ya kilimo na maeneo yaliyotengwa kwaajili ya kilimo yasitumike kwaajili ya mifugo.
"Ni lazima Kilimo chetu na Mifugo yetu iendane na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya maendeleo yetu" amesema Mkuu huyo wa Wilaya ya Malinyi.
Aidha, Mhe. Waryuba amewataka Wataalamu wa Kilimo Wilayani Malinyi waelimishe Wakulima kulima kilimo chenye tija kwa kulima eneo dogo lakini lenye uwezo wa kuzalisha zaidi.
Mhe Waryuba pia katika mkutano huo wa hadhara amewapongeza Wananchi wa Kata ya Biro kwa kuzalisha zao la pamba.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa sana Wilayani Malinyi kwa kuleta fedha katika miradi mikubwa na hivyo amewataka Wananchi wa Kata ya Biro kumuunga mkono Mhe. Rais kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika katika maeneo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.