Walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani malinyi wametakiwa kusimamia na kutekeleza mitaala iliyowekwa kwani ndiyo kazi kubwa na ndio wajibu wao.
Kauli hiyo imetolewa leo na afisa elimu mkoa morogoro BI EFLASIA BUCHUMA wakati wa kikao cha mazungumzo ambacho kimehusisha mkurugenzi mtendaji, maafisa elimu msingi na sekondari, waratibu elimu kata, walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari zote wilayani malinyi na wageni wengine mbalimbali ambao walialikwa katika ukumbi wa halmashauri.
Wakati akisoma taarifa fupi mbele ya afisa elimu mkoa, afisa elimu taaluma elimu sekondari James Msindo ameainisha changamoto mbalimbali zinazokabiri idara ya elimu msingi na ekondari kuwa hakuna usafiri wa uhakika, kukosekana kwa jengo la ofisi, hakuna shule hata moja inayotoa chakula cha mchana, na upungufu wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu huku mikakati waliyojiwekea ni kufaulisha kwa 85% katika mitihani ya taifa mwaka 2017, kuendelea kufuatilia utendajikazi wa walimu katika shule,kufanya uhamasishaji kwa jamii kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi.
Katika kikao hicho bi Buchuma amesema kuwa maelezo yote yanayotoka kwa viongozi ni vyema yakatekelezwa huku akiwapongeza walimu hao kwa ujumla kwa taarifa nzuri waliyoiandaa licha ya kuwa na chamgamoto kwani changamoto zilizopo wilaya ya malinyi zipo pia katika maeneo mengine mbalimbali hivyo wapange mikakati ya kujua namna gani ya kuweza kutatua changamoto hizo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Aidha ameongeza kuwa katika suala zima la kusimamia utoaji wa taaluma wanapaswa kujituma ipasavyo kwani kwa wastani wa matokeo ya darasa la saba 2016 hayakuwa mabaya kiwilaya kwa wstani wa 75.6% hivyo amewapongeza na kuwasisitiza kuwa wasiridhike na matokeo hayo kwani kitaaluma mkoa mzima bado unasuasua.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.