Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe . Sebastian Waryuba wakati akizungumza na Wananchi wa Kata hizo zilizojumuisha Kijiji cha Njiwa juu, Minazini, Alabama na Njiwa chini juu ya umuhimu wa Uhifadhi wa pori la Akiba la Kilombero B.
Wakiwasilisha hoja zao kwa Mkuu wa Wilaya Wananchi hao wameeleza kuwa maeneo hayo yaliyobainika kuwa yapo ndani ya pori la Akiba ndiko mahali wanapoishi na familia zao na ni maeneo wanayoyategemea kwa shughuli za kiuchumi na kilimo na kwamba endapo maeneo hayo yatabaki ndani ya pori la akiba Wilaya ya Malinyi haitakua na shughuli za kiuchumi zitakazotosheleza mahitaji ya Wananchi wake .
Kwa upande mwingine Wananchi hao wamelalamikia uzembe wa Viongozi wa Serikali za Vijiji kwa kugawa maeneo bila kuzingatia taratibu za ugawaji ardhi na kusababisha migogoro ya ardhi iliyopelekea Wananchi kwenda kuanzisha Makazi katika maeneo yaliyopitiwa na pori la akiba.
Akijibu hoja hizo, Mhe. Mkuu wa Wilaya amesema kuwa makusudio ya tangazo la Serikali GN namba 64 la tarehe 17/2/2023 ni kutunza vyanzo vya Maji, milima na Uhifadhi wa Mazingira ili vituwezezeshe kupata Maji ya uhakika na ya mwendelezo kuweza kulisha bwawa la Mwalimu Nyerere pasipo kukoma ili maendeleo yaendelee kuwepo kutokana na umeme utakaozalishwa mahali pale.
"Tangazo la Serikali ni Sheria na limetamka maeneo, sisi Kama Viongozi tuna wajibu wa kufuata na kuwaelimisha Wananchi kuhusu umuhimu wa jambo hili, Tangazo hili limepitia michakato yote sio jambo lililoibuka kutoka hewani" amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
"Nataka niwaambie ukweli, Mimi Sina kawaida ya kumung'unya maneno, Kama upo ndani ya eneo la pori la Akiba unatakiwa kuhama, hamia upande ulio nje ya pori la Akiba, kwa kuwa katika eneo hilo shughuli zote za Kilimo, ufugaji na ujenzi wa aina yoyote haziruhusiwi"amesema Mhe. Sebastian Waryuba
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kwa TAWA kuzingatia weledi, uaminifu na kutekeleza majukumu yao bila rushwa, na amewataka Wananchi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza jambo hilo na kuwaagiza Viongozi wa Serikali za Vijiji kuhakiksha kuwa Wananchi wote watakaohama kutoka pori la Akiba wanapatiwa maeneo ya kuishi katika Vijiji vilivyo nje ya mpaka wa pori la Akiba
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.