Mkuu wa wilaya ya malinyi majura kasika ameongeza awamu nyingine ya upigaji chapa ng’ombe wilayani malinyi kutokana na kuonekana kwa mifugo mingi kutokuwa na chapa.
Ameyaeleza hayo jana wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha ihowanja tarafa ya ngoheranga kilichofanyika katika ofisi ya serikali ya kijiji hicho.
Kasika amesema kuwa kitendo cha kutosajili mifugo ni kosa kisheria kwani itawia vigumu kutambua mifugo inayoweza kuingia kiholela katika wilaya yake hivyo ametoa onyo kwa wale ambao hawakupiga chapa mifugo watumie fursa hiyo kwani wasipofanya hivyo hawatotambulika kisheria na kuonekana ni mvamizi na atakuwa amejifukuzisha mwenyewe katika wilaya.
Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya imekuja mara baada ya kupata taarifa inayosemekana kuwa kuna mifugo zaidi ya 2000 imeingia kinyemela kutoka songea wakiwa wamepitia barabara itokayo kilosa kwa mpepo ndipo mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya na viongozi wengine wakawafatilia mifugo hiyo mbuga kwa mbuga takribani masaa 6 wakiwa mbugani lakini bila mafanikio.
Hata hivyo ametoa onyo kwa watendaji wa vijiji na uongozi wa vijiji kwa ujumla kama kuna wanaojihusisha na uingizwaji wa mifugo kiholela waache mara moja huku akiwataka wananchi wale walinzi kwa suala hili.
Zoezi la upigaji chapa limeshakamilika kwa awamu ya kwanza ambapo ng’ombe waliofanikiwa kupiga chapa ni 109,887. Na awamu ya pili mpaka sasa ng’ombe 230 tayari zoezi bado linaendelea huku lengo likiwa ni kuweza kutambua mifugo iliyopo na kuweza kuwatengea maeneo ya malisho kupunguza ili kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji inayoweza kujitokeza.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.