Wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya vijiji katika halmashauri ya wilaya ya Malinyi wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata weledi lasivyo wakirudia makosa kwa makusudi serikali itawachukulia hatua kali.Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wa Wilaya ya Malinyi Lameck Lusesa wakati Wa ufunguzi Wa mafunzo kwa mabaraza ya Ardhi ya vijiji kwa ajili ya kujenga uwezo katika utatuzi Wa migogoro ya ardhi.Mafunzo hayo kwa wajumbe wa vijiji nane wa tarafa ya Malinyi yanaendeshwa na wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi(LTSP).
Lusesa amesema serikali inatumia gharama kubwa kutoa mafunzo lakini kuna baadhi ya wajumbe kwa makusudi kabisa wanaona nafasi waliyopewa ya kusuluhisha migogoro ya Ardhi kwao imekuwa ni dili la kujipatia Fedha na kuonya kuwa baada ya kupatiwa mafunzo yeyote atakaebainika kupokea rushwa jela inamuita..Amebainisha kuwa kila siku katika ofisi ya Mkuu Wa Wilaya wananchi wanakuja kulalamika kuwa hawatendewi haki na wajumbe Wa mabaraza ya vijiji na yote hiyo inatokana na wajumbe kutoa maamuzi kwa upendeleo.
Naye Mwenyekiti Wa baraza La Ardhi katika Wilaya za Kilombero,Ulanga na Malinyi Roginamus Rugarabamu aliwataka viongozi wapya Wa vijiji wanaochaguliwa kuacha tabia ya kutengua maamuzi ya ugawaji Wa Ardhi uliofanywa na serikali zilizopita kwani maamuzi hayo ni halali kisheria na wao hawana mamlaka kutengua labda maamuzi ambayo hayakushirikisha wananchi.Aidha Rugarabamu amewataka wajumbe Wa mabaraza ambao wataona kesi wanazotaka kutoa maamuzi zina maslahi juu yao wajitoe mapema ili kutoivuruga kesi.
Kwa upande wake mtaalamu Wa Sheria toka LTSP James Balele alisema mafunzo hayo ni muendelezo Wa mafunzo kwa wajumbe Wa mabaraza ya vijiji na kata katika Wilaya tatu za mradi ambazo ni Kilombero,Ulanga na Malinyi.Balele amesema katika mafunzo hayo kwa wajumbe Wa mabaraza ya Ardhi ya vijiji katika Wilaya ya Malinyi yameanza katika tarafa ya Malinyi na kuendelea Ngoheranga na Mtimbira na yameanza Oktoba 17 na kumalizika novemba 3 mwaka huu.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.