Maneno hayo yamesemwa na mgeni rasmi wa siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16 juni Ndugu Rashidi Ally Kiding’a mwenyekiti wa PARALEGAL wilaya ambayo katika Wilaya hii ya Malinyi yameadhimishwa katika kata ya Ngoheranga nje ya mji wa Malinyi.
Akiongea na watoto, pamoja na wananchi wa tarafa hiyo ya Ngoheranga amewaasa wazazi kuwalea watoto katika maadili mema ili waweze kuwa raia wema na viongozi bora wa nchi yetu hapo baadae.Amewaeleza wazazi wana wajibu mkubwa wa kupinga ukatili mbalimbali dhidi ya watoto ,ikiwemo ndoa za utotoni, pia wana wajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu iliyobora ambayo ndo msingi wa maisha yao ya baadae.
Vilevile amewasihi wazazi kutowaficha watoto walemavu kwani wana haki sawa na watoto wengi, ya kupata elimu na malezi bora ili nao waweze kujitegemea katika maisha yao. Vilevile amewasihi watoto kupokewa yale mema wanayopewa na kuelekezwa na wazazi wao, kuwatii na kujituma.
Maadhimisho ya siku mtoto wa Afrika yanafanyika kila mwaka Afrika kwa kumbukumbu ya watoto wa kiafrika waliouawa kikatili katika kitongoji cha Soweto huko Afrika ya kusini walipoandamana kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa na makaburu dhidi ya waafrika.
Mwisho mgeni huyo alitoa zawadi kwa wanafunzi walioshiriki michezo mbalimbali katika maadhimisho hayo.
Kauli ya mwaka huu ni “Mtoto ni msingi wa Taifa Endelevu ,tumlinde na kumuendeleza”
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.