Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis amependezwa na hali ya uzalishaji wa mazao ya vipando katika Banda la Malinyi yaliyozalishwa kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Mhe. Shamata Shaame amesema teknolojia hizo zilizotumika katika vipando hivyo na kuleta uzalishaji mkubwa wa mazao zisambazwe katika maeneo mengine nchini ili Wakulima wanufaike na walime kilimo chenye tija.
Aidha, Waziri huyo wa Kilimo wa Zanzibar akiwa katika Banda la Malinyi aliiagiza Kampuni inayojishughulisha na kilimo Mzuri Afrika inayomiliki mashine ya kisasa ya Kilimo iitwayo Mzuri Pro-Til kuanzisha shamba darasa ili kutoa hamasa kwa Wakulima na Wananchi ili kujua uzuri na ufanisi wa teknolojia hiyo ya kisasa ya Kilimo.
"Teknolojia ikiwa nzuri hakuna shida, Kila mtu atataka kuitumia hata Kama ni gharama kiasi Gani. amesema Mhe. Shamata Shaame."
Mhe.Shamata Shaame pia amesema kuwa anafarijika sana kuona Watanzania wanapopata nafasi ya kujifunza teknolojia nzuri nchi na makampuni mengine duniani lakini mwisho wa siku wanakumbuka kuleta teknolojia hizo nyumbani na kuongeza kuwa huo ndio uzalendo unaotakiwa wa kuipenda nchi yetu kwa vitendo.
Mashine hiyo ya Kilimo Ina uwezo wa kulima ekari saba na nusu ndani ya saa Moja, na inafanya kazi ya kulima, kulegeza udongo, kuweka mbolea na kuweka mbegu aridhini kwa wakati mmoja.
Maonesho haya ya Nanenane yanayoendelea Mkoani Morogoro yanashirikisha Taasisi mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ambapo Malinyi inashiriki kutoa Elimu kuhusu teknolojia mbalimbali za Kilimo.
"VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.