Akizungumzia kuhusu changamoto ya lishe duni, kukosa ujuzi wa stadi za maisha, kukatisha masomo, vifo katika umri mdogo, na mimba katika umri mdogo, amesema husababishwa na uelewa hafifu wa afua za afya zinazowahusu vijana ikiwa ni pamoja na afua za kujikinga na kutokujua mahali pa kwenda kwa huduma na taarifa sahihi.
Aidha, kuhusu ukatili dhidi ya watoto na ukatili wa kijinsia, Bi Rehema Rajabu amesema kuwa ni wajibu wa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuwalinda watoto na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kutumia vyombo mbalimbali kutoa taarifa dhidi ya ukatili ikiwemo Polisi, Dawati la jinsia na kwa Wanafunzi watoe taarifa kwa Mwalimu/Waalimu ili kupunguza na kumaliza kabisa ukatili katika jamii.
Bi Rehema Rajabu ameongeza kuwa, Kwa kutambua umuhimu na mchango mkubwa wa vijana katika Taifa letu, Serikali kupitia sekta mbalimbali imefanya jitihada kubwa katika kuimarisha upatikani na utoaji wa huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana ambapo vituo 901 vinatoa huduma hizi nchini na vituo 177 vimetenga chumba maalum kwa ajili ya huduma ya afya ya uzazi kwa vijana.
KAULI MBIU :
Afya ya uzazi :AFYA YANGU MAISHA YANGU
Siku ya Mtoto wa Afrika : ZINGATIA USALAMA WA MTOTO KATIKA ULIMWENGU WA KIDIGITALI
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.