Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba amefungua Mafunzo Elekezi kwa Waheshimiwa Madiwani. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri tarehe 5 Oktoba 2025.
Mafunzo hayo elekezi kwa Waheshimiwa Madiwani yametolewa na Wataalamu Wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa- Hombolo.Waheshimiwa Madiwani wamefundishwa Mada mbalimbali kama Uongozi na Utawala Bora, Sheria za Uendeshaji wa Shughuli za Mamlaks za Serikali za Mitaa, Muundo, Majukumu na Madaraka ya Serikali za Mitaa,Uendeshaji wa Vikao na Mikutano katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akifungua Mafunzo hayo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi alitoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Mafunzo ya Madiwani. Mheshimiwa DC Waryuba amesema Mafunzo Elekezi kwa Waheshimiwa Madiwani ni Mafunzo muhimu kwani elimu haina mwisho. Na amewaeleza Waheshimiwa Madiwani kuwa wao ndio "Engine" ya Halmashauri wakiwa vipofu na viziwi Halmashauri haitaenda na Halmashauri yoyote inayo "perform" lazima iwe na ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji,Wataalamu na DC. Hivyo anataka kuona Halmashauri yenye mabadiliko chanya.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.