Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi yazindua Ugawaji na Upandaji wa Miche ya Michikichi na Kakao. Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba tarehe 7 Januari 2026. Ikiwa ni Ishara ya kutekeleza azma ya Mkoa wa Morogoro ya kuwa na mazao ya mkakati yatakayoweza kuinua Uchumi wa Wakulima na kuongeza pato la Halmashauri. Halmashauri ya Malinyi ina mazao 4 ya kimkakati ambayo ni Korosho, Michikichi, Kakao na Embe ambayo kigezo cha kuyachagua mazao hayo ni matakwa na mahitaji ya Wakulima wengi na hali ya Kiikolojia( Hali ya Kimazingira ya Malinyi)
Akizindua ugawaji wa Miche ya Michikichi na Kakao DC Waryuba ameipongeza Halmashauri kwa Uanzishwaji wa Shamba Darasa na matokeo yake yanaonekana kwani Wananchi wanapata manufaa wakiwa Malinyi badala ya kusubiria kipindi cha Maonesho ya Nane Nane Morogoro. Jumla ya Miche 50,000 ya Korosho na 17343 ya Chikichi imegawiwa kwa Wakulima na usambazaji wa Miche 20,000 ya Kakao na upandaji unaendelea.
Mheshimiwa DC Waryuba amewataka Wataalamu wafanye utafiti kutokana na mazao yanayohimili hali ya hewa ya Malinyi na kawataka watoe Elimu kwa Wakulima kuhusu zao la Maembe kwani Maembe ya Malinyi ni mazuri kwa biashara. Pia ametoa Shukrani kwa Wataalamu, Wilaya ya Malinyi ndio inaongoza kwa uzalishaji wa Koroshi kwa Mkoa wa Morogoro kwa sababu Ardhi ya Malinyi inakubali, kwa upande wa Zao la Kakao zao hilo lina bei nzuri hivyo amewataka Wakulima walichangamkie.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.