Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Moses Chogo tarehe 5 Desemba 2025 imekabidhi gari la Wagonjwa kwa kituo cha Afya cha Ngoheranga, Kifaa Tiba cha "BIOSAFETY CARBINATE" Kifaa kinachokinga Mtoa huduma dhidi ya vimelea vinavyoambukizwa kwa njia ya hewa wakati wa upimaji wa Sampuli kilichotolewa kwa Ufadhili wa Shirika la SolidarMed na imegawa Mahitaji ya wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Malinyi.
Akikabidhi Vifaa hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Moses Chogo ameutaka Uongozi wa Hospitali ya Wilays kuhakikisha unatunza vifaa hivyo kwa manufaa ya muda mrefu. Pia amelitakaBaraza la Madiwani liitangaze Hospitali ya Wilaya ya Malinyi kwani Watumishi wapo wa kutosha. Vilevile Mh.Mwenyekiti amesisitiza anahitaji mahusiano mazuri kati ya Baraza na Watumishi wa Halmashauri kwani bila mahusiano mazuri unaweza kuharibu kwa Jamii na amewataka Watumishi wawe na kauli nzuri kwa Wagonjwa na Viongozi.
Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) Dk. Julius Nyasongo amesema Kifaa Tiba cha "BIOSAFETY CARBINATE" na Gari la Wagonjwa (Ambulance) vitasaidia kuongeza kasi ya huduma kwa Wananchi. Dk. Nyasongo amesema Wananchi wa Malinyi wanafurahia uboreshwaji wa huduma zinazotolewa kwenye Hospitali za Serikali.
Kwa upande wa Mganga Mwanzilishi wa Hospitali ya Wilaya Dk. Marwa Mikwabe amesema huduma za Hospitali zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa sambamba na ongezeko la Watumishi wake. Hospitali hiyo ya Wilaya ilianza na Watumishi 12 hivi sasa ina Watumishi zaidi ya 100 na imepata vifaa Tiba vingi kutoka Serikali.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.