Tarehe 04/12/2025 kupitia Mkutano wa kwanza wa Halmashauri, Madiwani waliochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba,2025 wameapishwa rasmi na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Malinyi Ndugu James Clement Mwakalosi zoezi lililoenda sambamba na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
Kufuatia Uchaguzi huo Mheshimiwa Moses Martin Chogo Diwani wa Kata ya Igawa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kupata Kura zote 15 zilizopigwa huku Mheshimiwa Liko Venance Likomo Diwani wa Kata ya Sofi kupitia CCM amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata Kura 13 kati ya 15 ambapo Kura 2 ziliharibika.
Zoezi hilo lilisimamiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Malinyi Ndugu Saida Abbas Mhanga ambapo amewataka Madiwani kufanya kazi kwa Umoja, Upendo na Ushirikiano baina ya Madiwani na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Khamis Katimba na watatue kero za Wananchi bila ya Ubaguzi.
Kuapishwa kwa Waheshimiwa Madiwani pamoja na kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti sambamba na kuunda Kamati za Kudumu za Halmashauri ni hatua ya kuanza kutekeleza majukumu ya Baraza katika Halmashauri kwenye kuwatumikia Wananchi wa Malinyi.
Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi linaundwa na Madiwani 14 ambao ni Mh.Moses Martin Chogo, Mh.Liko Venance Likomo, Mh.Raina Paulo Mbelembo,Mh. Editha Ally Makumba, Mh.Stahili Yusuph Kiponda, Mh.Aloycia Likanda, Mh.Ditric Dismas Makolela, Mh. Christensia Peter Nyela, Mh.Doglas Ulaya Mhali, Mh.Jestas Jonas Kyerike, Mh.Bonaventura Killian Kiwanga, Mh.Festus Saulo Vundwe, Mh. Maina Juma Mrisho na Mbunge wa Jimbo la Malinyi Mh.Dk, Mecktridis Fratern Mdaku.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.