Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Malinyi Ndugu Khamis Katimba akisalimiana na mmoja wa Wakazi wa Kata ya Mtimbira aliyefika katika kituo cha kujiandikishia Shule ya msingi Mtimbira kwaajili ya kuhakiki taarifa zake mapema jana Mei 16, 2025 ikiwa ni awamu ya pili ya zoezi hilo.
Katimba alitembelea vituo kadhaa katika Jimbo la Malinyi ili kujionea zoezi la uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga kura katika Jimbo hilo linavyoendelea.
Ndugu Katimba ametoa Wito kwa Wakazi wa Jimbo la Malinyi ambao hawajajiandikisha kujitokeza katika awamu hii ya pili ili waweze kujiandikisha, na wale ambao waliokwishajiandikisha katika awamu ya kwanza wafike katika vituo vilivyo karibu na maeneo yqo ili waweze kuhakiki taarifa zao na hatimaye kuitumia haki yao ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2025.
"KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.