Afisa Mwandikishaji Jimbo la Malinyi Ndugu Khamis Katimba akifungua mafunzo ya siku moja kwa Watendaji wa uboreshaji daftari la kudumu la Wapiga kura awamu ya pili ngazi ya Kata, Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo Misegese.
Katimba amewataka Watendaji hao kujiepusha na vitendo visivyofaa na badala yake kufanya kazi hiyo kwa bidii zaidi ili kazi hiyo iweze kutoa matokeo yaliyo bora zaidi kwakuwa Watendaji hao hao tayari wana uzoefu kutokana na zoezi la uandikishaji lililofanyika mwezi machi 2025.
Zoezi la uboreshaji daftari la Wapiga kura Jimbo la Malinyi linatarajiwa kuanza tarehe 16 Mei, 2025 na litakamilika tarehe 22 Mei 2025 ambapo Wakazi wa Jimbo la Malinyi watapata nafi ya kuhakiki taarifa zao, kujiandikisha, kuhamisha taarifa zao pamoja na kuondoa kwenye daftari Wapiga kura waliopoteza sifa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.