Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi tarehe 15 Januari 2026 imekagua utekelezaji wa Miradi yenye thamani ya takribani Shillingi Millioni 954,800,000 ikiwa ni Fedha za Mapato ya Ndani na Fedha kutoka Serikali Kuu.
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango inaongozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Moses Chogo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi na Makamu wake Mheshimiwa Liko Venance Likomo Diwani wa Kata ya Sofi, imepata fursa ya kutembelea na kukagua miradi kama ifuatavyo:-
Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Upasuaji Mkubwa (Theatre) wa Hospitali ya Wilaya ambapo ujenzi upo kwenye hatua za upauaji, Kamati imekagua ukamilishaji wa Stendi Kuu ya Mabasi iliyopo Misegese ambapo kazi ya ujazaji kifusi awamu ya kwanza imekamilika. Kamati imejiridhisha na ujenzi kwa sababu Stendi hiyo ni jicho la Madiwani kwa kuwa ni Chanzo cha Mapato ya Halmashauri na pia ni huduma kwa Wananchi wa Malinyi.
Kamati imekagua Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji (DED) ambayo ipo kwenye hatua ya umaliziaji. Kamati pia imetembelea eneo la upimaji wa Viwanja na ulipaji wa fidia eneo la Nyangali ambalo lina ukubwa wa ekari 36.48 na viwanja vilivyopimwa vipo 166 na gharama ya fidia ni Shilingi Millioni 99 na kila mkazi wa eneo hilo atapewa kiwanja kimoja.
Kamati imetembelea Ujenzi wa Madarasa Mawili na matundu sita ys vyoo katika Shule ya Awali Majiji ambapo madarasa yamepauliwa na matundu ya vyoo yapo kwenye hatua ya ripu na uzio upo hatua ya ukuta. Kamati imeomba ubora uzingatiwe katika ukamilishaji wa ujenzi na imeomba dokumenti za umiliki wa Ardhi zipatikane kwa wakati ili hata kama Mradi utatembelewa na Mbio za Mwenge kusiwe na kasoro yoyote.
Mwisho Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ilimaliza Ziara yake kwa kutembelea Shule ya Msingi Kiswago ambapo Jengo lenye Madarasa Matatu na Ofisi ya Walimu Paa lake limeezuliwa na upepo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.