Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi tarehe 24 Januari 2026 limefanya Mkutano wake wa kawaida katika Ukumbi wa Halmashauri na limepitisha taarifa za Kamati za Robo ya Pili kwa Mwaka 2025/2026.
Taarifa za Kamati zilizowasilishwa na Wenyeviti wa Kamati na kupitishwa na Baraza la Madiwani ni kama ifuatavyo:-
Kamati ya UKIMWI, Kamati ya Huduma za Afya na Elimu, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Moses Chogo alitoa pongezi kwa Wenyeviti kwa uwasilishaji wao mzuri wa taarifa za Kamati. Pia alisisitiza kuhusu uhamasishaji wa uandikishaji wa Wanafunzi kuanzia Elimu ya Awali, Msingi mpaka Sekondari na ameagiza Watoto waendelee kuandikishwa Mashuleni mpaka mwezi Machi.
Mheshimiwa Moses Chogo ametoa agizo kwa Taasisi mbalimbali za Umma zinazotoa huduma ndani ya Halmashauri ya Malinyi kama TANESCO, TARURA na RUWASA nazo ziwe zinawasilisha kwenye Baraza la Madiwani taarifa zao za Utekelezaji wa majukumu yao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.