Katibu Tawala Wilaya ya Malinyi ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Wilaya Ndugu Saida Abbas Mhanga amefungua Ligi ya Mpira wa Miguu ya Amani Cup tarehe 14 Oktoba 2025.
Ligi hii ya Amani Cup inachezwa katika Uwanja wa Misegese uliopo jirani na Benki ya NMB eneo la Njiapanda, na inahusisha timu sita ambazo ni Msamvu Road FC, Watumishi FC, New Fighter FC, Ngozi Kunoga FC, Challenge FC na Igawa FC.
Katika Mchezo wa Ufunguzi ulizikutanisha timu za Msamvu Road vs Watumishi FC ambapo mechi iliisha kwa matokeo ya Suluhu ya bila kufungana (0-0)
Katika neno lake la Ufunguzi Katibu Tawala Ndugu Saida Abbas Mhanga aliwasihi Wachezaji kucheza kwa Amani na Usalama.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.