Katibu Tawala Wilaya ya Malinyi Ndugu Saida Abbas Mhanga amewaongoza Wana Malinyi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mazingira Duniani. Maadhimisho hayo katika Wilaya ya Malinyi yameadhimishwa Kijiji cha Majiji Kata ya Sofi, Tarafa ya Mtimbira tarehe 26 Septemba 2025.
DAS Mhanga alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba. Kauli Mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Afya ya Mazingira Duniani ni "Tokomeza taka za Plastiki jenga jamii yenye Afya bora"
Mapema asubuhi DAS Mhanga alipata nafasi ya kushirikiana na wenyeji wakazi wa kijiji cha Majiji kufanya usafi na kuzoa taka. Katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Hadhara DAS Mhanga aliihamasisha jamii kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaopelekea kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.
DAS Mhanga amesema katika kuadhimisha siku ya Afya ya Mazingira tunakumbushwa kila taka kuwa ina thamani endapo tutaiona kwa jicho sahihi mfano Plastiki zinaweza kutengeneza vigae, mapipa au vifaa vya matumizi nyumbani. Mabaki ya Chakula yanaweza kubadilishwa kuwa mbolea na kutengeneza rutuba ya Udongo. Taka ngumu zinaweza kuzalisha nishati mbadala na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.
DAS Mhanga alitoa maelekezo kama ifuatavyo:-
1.Kila Kijiji kiwe na Sheria ndogo za Usafi wa Mazingira.
2.Kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na kamati ya Usafi wa Mazingira.
3.Kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Kamati ya Usafi na Mazingira.
4.Kila Kijiji kiwe kinashiriki ukusanyaji wa taka ili kudhibiti kuzagaa kwa taka ngumu.
5.Wananchi waepuke kutupa plastiki ovyo.
6.Kuwafuatilia Wananchi wasio na vyoo.
Kabla ya hotuba ya Mgeni Rasmi, Ndugu Benard Mbumbumbu Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu alipata wasaa wa kutoa Elimu ya Kampeni ya Choo Bora kwa kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo.
Kauli mbiu inasema " Usichukulie Poa nyumba ni Choo" Kwa Wilaya ya Malinyi takwimu zinaonesha Asilimia 52% ya wakazi wanatumia vyoo bora, Asilimia 46% vyoo vya shimo na Asilimia 2% hawana vyoo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.