Katibu Tawala Wilaya ya Malinyi Ndugu Saida Abbas Mhanga amewaongoza Wauguzi wa Mkoa wa Morogoro kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Sebastian Waryuba. Sherehe hizo Kimkoa zimeadhimishwa Wilaya ya Malinyi kwenye kiwanja cha Shule ya Msingi Nawigo tarehe 25 Julai 2025.
Siku ya Wauguzi Duniani ni Kumbukizi ya Florence Nightngale Mwanzilishi na Muasisi wa Siku ya Wauguzi. Kauli mbiu ya Mwaka huu ni"Wauguzi nguvu ya Mabadiliko Duniani" DAS Mhanga alitoa Salamu za dhati kutoka kwa Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan na kutambua jitihada za Wauguzi na Jitihada za Serikali iliyoweka Mazingira Mazuri na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
DAS Mhanga aliagiza Wakurugenzi waajiri Wauguzi kwa kutumia Mapato ya ndani ili kupunguza uhaba wa Wauguzi kwani asilimia 80% katika Sekta ya Afya inabebwa na Wauguzi/Muuguzi anahusika. Amewaomba waendelee kufanya mafunzo kazini na wakumbuke kuhuisha Leseni zao.
DAS Mhanga amewaomba Wauguzi katika kazi zao wamtangulize Mungu mbele, wapendane,washirikiane na wasaidisne.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.