Katibu Tawala Wilaya ya Malinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Saida Abbas Mhanga amefunga kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba Ligi ya Mpira wa Miguu ya Amani Cup tarehe 25 Oktoba 2025.
Mchezo wa Fainali umezikutanisha timu za New Fighter vs Ngozi Kunoga ambapo mchezo uliisha kwa Ngozi Kunoga kuibuka na Ushindi wa goli 1-0 na kufanikiwa kubeba kitita cha Fedha Shillingi 250,000/=, Mshindi wa Pilu New Fighter alipata kitita cha Fedha Shillingi 150,000/= na Mshindi wa Tatu wa Mashindano hayo Msamvu FC waliibuka na kitita cha Shillingi 100,000/=
Katika neno lake la kufunga Mashindano DAS Saida Mhanga alimshukuru Muandaaji wa Mashindano kwa kuhakikisha Michezo inapaa ndani ya Wilaya ya Malinyi na kutoa vipaji na amewaomba Wachezaji wakawe Mabalozi wajitokeze wakapige Kura tarehe 29 Oktoba 2025.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Katimba ameahidi kushirikiana na Wana Malinyi kwenye Mabonanza na Jogging huku akiahidi uwepo wa Bonanza la kuwashukuru Wananchi baada ya Uchaguzi Mkuu huku akiwaomba Washiriki wote wajitokeze kupiga Kura ya Rais,Mbunge na Madiwani tarehe 29 Oktoba 2025.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.