Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Wakili Msomi Mheshimiwa Sebastian Waryuba amefungua Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo Robo ya Kwanza Julai=Septemba 2025. Kikao hicho kimefanyika tarehe 4 Oktoba 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Malinyi.
Katika Kikao hicho cha cha Tathmini Mada mbalimbali zilijadiliwa kuhusu Kilimo na Mifugo, Maendeleo ya Jamii, Manunuzi, Sheria, Tathmini na Ufuatiliaji, Fedha na Uhasibu, Afya=Saratani ya Matiti, TAKUKURU-Utawala Bora, Uhamiaji, Polisi, Misitu-TFS, Barabara-TARURA, Maji-RUWASA.
Katika hotuba yake ya Ufunguzi Mheshimiwa DC alitoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpatia kipande cha Malinyi akisimamie kama Mkuu wa Wilaya.
Mheshimiwa DC Waryuba alimpongeza DED Katimba kwa uthubutu wake wa kutengeneza Magari mabovu ya Halmashauri na amemtaka DED Katimba na Afisa Usafirishaji (TO) wasiwavumilie madereva wazembe huku akisisitiza dhana ya Kisheria ya "Contributory Negligence" Dereva aliyesababisha Uzembe, Uharibifu na hasara afidie kulipa akisema Utamaduni huu ukitengenezwa na kutumika utasaidia.
Mheshimiwa DC Waryuba amewataka Madereva wawe waadilifu na wafanyiwe Vetting, na hataki kusikia ajali za hovyo hovyo, waendeshe kwa spidi ya kawaida sio kali.
Mheshimiwa DC pia ameagiza Watu wa AMCOS washirikishwe kwenye Vikao vya Halmashauri.
Mheshimiwa DC Waryuba aligusia suala la Uwekezaji Malinyi mfano Kilosa Mpepo na dhana ya Kisheria ya "Mutatis Mutandis means Making necessary adjustments or changes to suit the specific situation" Kama kuna Wawekezaji waliopewa Ardhi kuwekeza na hawakuwekeza basi Ardhi hiyo irudishwe Serikalini.
Mheshimiwa DC Waryuba alimuomba DED Katimba atafute maeneo atengeneze Ranchi au atafute Mwekezaji atengeneze Ranchi kwa ajili ya Ufugaji akisema Ranchi itasaidia kuondoa migogoro ya Wakulima na Wafugaji.
Mheshimiwa DC Waryuba amewaomba Watendaji wa Kata na Vijiji wafuatilie Ushirika katika maeneo yao na amewaambia Watumishi wa Umma hawazuiwi kushiriki kwenye Ushirika.
Mheshimiwa DC Waryuba amemuagiza DED Katimba atume timu yake kusuluhisha migogoro ya mipaka kati ya Vijiji mfano Igawa na Biro.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.