Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba ameongoza Kikao cha Jukwaa la Maridhiano Wilaya ya Malinyi. Kikao hiko kimefanyika tarehe 2 Desemba 2025 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Jukwaa la Maridhiano na Amani linaundwa na Makundi mbalimbali kama Viongozi wa Dini, Vijana Maarufu, Wazee Maarufu, Sungusungu, Tiba Asilia, Wanawake,Wafanyabiashara, Wakulima,Wafugaji,Vyama vya Siasa nk. Kikao hiko pia kimehudhuriwa na DED Khamis Katimba, DAS Saida Mhanga na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Katika Kikao hiko Mheshimiwa DC Waryubs alitoa Shukrani za dhati kwa kuwa Uchaguzi Wilayani Malinyi umefanyika kwa Amani na Umeisha salama hivyo ameyashukuru Makundi yote ya Wananchi pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kuhakikisha Wilaya ya Malinyi ipo Salama.
Mheshimiwa DC Waryuba amesema yeye binafsi akiwa mteule wa Rais habagui Mtu yoyote kwa Dini,Kabila, Ufupi,Urefu,au Chama Chochote. Amewaomba Viongozi wa Dini wawafikishie Ujumbe Waumini wao kuhusu Amani Siku ya Ijumaa kwa Waislamu, Jumamosi Wasabato na Jumapili kwa Wakristo wa madhehebu yote. Mheshimiwa DC Waryuba amewaomba wawe mabalozi kwa Waumini, tupinge hamasa za Uchochezi wa fujo hakuna anayependa kuishi kwenye Shida, Hakuna asiyependa Amani.
Mheshimiwa DC Waryuba amesema Maisha yetu yapo kwenye Hatma yetu, Maisha ya Vijana yapo kwenye hatma zao. Hakuna Mtu wa Nje anayejua Shida za Watu wa Malinyi bali Wana Malinyi watazitatua wenyewe hivyo "Tuhubiri Amani kwenda mbele tufanye Shughuli zetu vizuri mambo yakiharibika hatuna pa kwenda. Ninaomba Ndugu zangu tudumishe Amani" alisema DC Waryuba.
DC Waryuba ametoa Kauli Mbiu ya "Amani iwepo Malinyi na Malinyi iwepo Amani"
Kwa upande wa DED Khamis Katimba amewaomba Viongozi wa Dini wawaelimishe Waumini wao wawe wanashiriki kwenye Shughuli za Miradi ya Maendeleo za Nguvu kazi kama kuweka vifusi,kuchimba msingi nk. Pia ameongelea Mikopo ya Asilimia Kumi(10%) kwa Waliokwisha Faidika na Mikopo hiyo wakumbuke kurudisha ili iweze kuwanufaisha Wananchi wengi. Mwisho DED Khamis Katimba amewaalika Wananchi kuhudhuria kwenye Ufunguzi wa Baraza la Halmashauri Siku ya Alhamisi tarehe 4 Desemba 2025.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.