Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba ameongoza kikao cha Baraza la Biashara Ngazi ya Wilaya. Kikao hicho kimefanyika tarehe 07 Oktoba 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi. Kikao hicho kinaundwa na Wajumbe wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Katika hotuba yake Mheshimiwa DC Waryuba alisema Vikao vya Baraza la Biashara vinapangwa ili kuleta "Mediation" Upatanishi na Usuluhishi kati ya Sekta ya Umma na Binafsi. Mheshimiwa DC Waryuba amesema kama kuna Changamoto yoyote katika Sekta Binafsi mfano Leseni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania "TRA". Wahusika kutoka Sekta ya Umma wanapokea malalamiko au changamoto na kutoa majibu,maazimio na maelekezo na Wajumbe wote kutoka Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wana kuwa na hadhi sawa ndani ya Kikao.
Katika Kikao hiko Mheshimiwa DC Waryuba alitoa maelekezo na maazimio kama ifuatavyo;
Amewataka Watu wa Ushirika watoe mafunzo na yaende kwa lugha wanayo ielewa(Lugha yao). Na anataka Spidi kwenye mafunzo yafanyike kwa Vyama vya Msingi.
Ametaka Wakala wa Vipimo(WMA) waandikiwe barua ili wakasimishe madaraka kwa Halmashauri.
Amewataka Wafanyabiashara wadhibitiane, waache wizi kwenye vipimo na mafuta.
Ameagiza Bodaboda wapewe mafunzo.
Ameagiza Wakulima wakajisajili ili waweze kupata Pembejeo (Mbegu Boram Viuatilifu na Mbolea) kwa utaratibu uliowekwa na Serikali.
Tanesco itoe ufafanuzi wa "Tarrif) na "Service Charges" na Elimu itolewe kwa Wananchi.
TRA watoe elimu ya mlipa kodi kwa Wananchi.
Wananchi watunze vyanzo vya Maji ili bwawa la Mwalimu Nyerere liweze kupokea Maji.
Maonesho ya Nane Nane mwakani yaoneshwe ndani ya Wilaya kabla ya kuanza kwa Maonesho ya Kanda ya Mashariki Morogoro.
Halmashauri iangalie namna ya kuanzisha Redio Malinyi "Local Radio"
Mwisho amesema milango iko wazi kwenda kwake na kwa Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Khamis Katimba.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.