Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba ameongoza Kikao cha Jukwaa la Maridhiano Wilaya ya Malinyi. Kikao hiko kimefanyika tarehe 23 Oktoba 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri.
Jukwaa la Maridhiano na Amani linaundwa na Viongozi wa Dini, Vijana Maarufu, Bodaboda, Sungusungu, Tiba Asilia, Wanawake,Wafanyabiashara, Wakulima, Wafugaji, Wafanyakazi nk.
Katika Kikao hiko Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alitoa Shukrani kwa Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kwa kumpa kipande cha Malinyi akisimamie na Shukrani kwa Watumishi wa Umma wakiongozwa na DAS Saida Mhanga na DED Khamis Katimba.
Katika Kikao hiko DC Waryuba alitoa Maelekezo kama ifuatavyo;
Ukatili wa Kijinsia ukemewe na kupigwa vita kwenye Nyumba za Ibada.
Mila na desturi mbaya zikemewe mfano Chagulaga na Ushoga.
Jamii itengeneze Kizazi cha kurithishana mazuri, watoto wadogo chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kwenda kwenye sherehe za usiku na Mwisho wa Sherehe iwe saa sita usiku.
Video za Matusi (Ngono) haziruhusiwi kuonyeshwa Mabandani hivyo Watu wa Utamaduni wafuatilie.
Viongozi wa Dini kuu mbili Wakristo na Waislamu wawafikishie ujumbe Waumini wao Siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuhusu umuhimu wa Amani.
Kuendesha danguro ni kosa kisheria.
Katika Kikao hicho Wadau wa Jukwaa la Maridhiano na Amani walitoka na Maazimio ( Tamko) yaliyosomwa na Katibu wa Jukwaa la Maridhiano na Amani Wilaya ya Malinyi Ndugu Baguwa Salum Kiwawite kama ifuatavyo;
1.Wanaunga Mkono Kauli Mbiu ya Malinyi Moja kabla ya Uchaguzi na Malinyi Moja baada ya Uchaguzi.
2.Wataendelea kuhamasisha Amani na Utulivu.
3,Watahamasisha maadili mema.
4.Wamekataa maandamano ya kwenye Mitandao.
5.Wanahamasisha Wananchi kujitokeza kwa Wingi kupiga Kura.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.