Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba amefungua Kikao kazi cha Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Kilimo,Mifugo, Uvuvi na Ushirika wa Mkoa wa Morogoro. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi tarehe 20 Novemba 2025.
Katika Kikao hiko Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alielezea mambo yafuatayo
Amewataka Wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika wasijiweke mbali (pembeni) bali wajiamini na kutenda na kama kuna changamoto wazidhibiti.
DC Waryuba ametoa Rai kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro kufanikisha zoezi la Kampeni ya Chanjo ya Mifugo kwa kadri ya Idadi ya Chanjo zilizotolewa.
Mheshimiwa DC Waryuba amesema Uvuvi Haramu umekithiri katika Bonde la Kilombero hivyo ametoa Rai kwa Mamlaka ya TAWA na Halmashauri zichukue hatua.
Mheshimiwa DC amesema Wizara ya Kilimo imetoa Vifaa vya kupima Afya ya Udongo hivyo ameomba kasi ya Upimaji Afya ya Udongo iongezeke.
Mheshimiwa DC Waryuba amewataka Wataalamu wawe na uwezo na ubunifu kushauri Chama Kikuu (UKICU) kianzishe Viwanda ili viweze kuchakata mazao ghafi ili kuyaongezea thamani na kuongeza Ajira kabla ya kuyauza nje ya Nchi.
Kikao kazi hicho kimejadili na kufanya tathmini kuhusu taarifa zifuatazo;
Taarifa ya Utabiri wa Hali ya Hewa,Taarifa ya Utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, Taarifa ya Utekelezaji wa Mazao ya Kimkakati, Taarifa ya Usajili wa Wakulima kwenye mfumo wa Utoaji wa Ruzuku wa Mbegu Bora za Mahindi na Wasilisho la Agenda 10/30 Kilimo ni Biashara.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.