Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Masuala ya Afya Ndugu Paul Chaote ambaye ni Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu (Afya) na Ujumbe wake wamefanya Ziara Wilaya ya Malinyi tarehe 18 Novemba 2025.
Ujumbe huo umekagua Miradi mbalimbali na umefanya ukaguzi wa hali ya utoaji wa Huduma katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kama vile Ujenzi wa Jengo la Upasuaji (Theatre), Jengo la kuhifadhi Maiti (Mortuary), Kichoma Taka(Incirator), Jengo la Utawala, Ward ya Watoto, Ward ya Wazazi,Phamacy, Stoo,Huduma za Matibabu, Ustawi wa Jamii, Masuala ya Utumishi na Utawala, Bima ya Afya(NHIF), Masuala ya Fedha, Matumizi ya Mifumo na Lishe.
Ndugu Chaote ameomba kuwe na Ushirikiano katika ngazi zote kwenye kukamilisha Miradi kuanzia ngazi ya Manunuzi wazingatie Ubora wa Vifaa(Standard). Kwa Upande wa "Walkway" amesema ujenzi wa jengo la Upasuaji"Theatre" unaweza kuendelea huku Mhandisi Mjenzi na Mhandisi wa Mkoa waone jinsi ya kuyazuia maji kwenye Walkway.
Kwa upande wa DED Khamis Katimba amesema amepokea maelekezo na wamepata Millioni 200 kwa ajili ya jengo la Theatre na ili jengo likamilike inahitajika Millioni 255. Na ameahidi mpaka mwezi Desemba Jengo litakamilika.
Vilevile DED Khamis Katimba ameahidi yeye binafsi atafanya Ziara Hospitali ya Wilaya na atakutana na CHMT ya Afya na ameahidi atayafanyia kazi maelekezo na ushauri uliotolewa kwenye Ziara hiyo ya Ukaguzi wa Hospitali.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.