Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba amewaongoza Walimu wa Shule za Msingi Wilaya ya Malinyi kwenye Hafla(Tafrija) ya kuwapongeza Walimu kwa Ufaulu mzuri wa matokeo ya Darasa la Saba 2025 kwa kushika nafasi ya kwanza Mkoa wa Morogoro. Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nawigo tarehe 29 Novemba 2025.
Hafla hiyo ilipambwa na Burudani na Matukio mbalimbali kama kucheza kwaito,Mashairi,Dua na Sala, Kukata Keki Shampeni ambapo Shule 10 Bora zilitambulishwa ambapo Walimu waliotoa A nyingi walipewa Barua za pongezi na Pesa Taslimu.
Katika hotuba yake Mheshimiwa DC ametoa pongezi kwa Mheshimiwa Mbunge, Mkurugenzi wa Halmashauri na Walimu wote 469 wa Shule za Awali na Msingi na Wazazi. Ambapo amesema Walimu wametekeleza Mkakati walioupanga pamoja ndio maana matokeo yamekuwa mazuri. Amesisitiza Walimu wanahitaji Pongezi kwani kuyahamisha Maarifa kwenda kwa Mtoto Mdogo siyo jambo dogo.
DC Waryuba alielezea dhana ya Uelewa ya "Mwalimu ni Ualimu na Ualimu ni Mwalimu" na ametaka Watoto wale vyakula vyenye virutubisho ili waweze kushika mambo kwa haraka. Na amesema Suala la Chakula Shuleni Sio la Hiari, Na anataka mikakati iwepo pia kwa upande wa Sekondari ili nao wafaulishe vizuri kams Msingi.
Kwa upande wa somo la Hisabati DC Waryuba amesema yeye ni Bingwa hivyo anataka akutane na Walimu wa Hisabati awape mbinu za kufundisha ili Mwanafunzi aelewe Hisabati.
"Tunaposema Hongereni, tunawabariki ili msonge mbele, Hongereni Walimu wangu" alisema DC Waryuba. Na amesisitiza suala la Amani tuilinde Amani ya Nchi yetu kama "DHAHABU" tupendane, tusibaguane kwa Dini, Rangi au Kabila.
Kwa upande wa Mbunge Mheshimiwa Mecktrids Mdaku amesema Walimu anawathamini, anawapenda, na yupo pamoja nao, atashirikiana na Walimu kwa hali na mali na ameahidi atafanya Kikao na Walimu wote ambapo kwenye Hafla hiyo Mheshimiwa Mbunge amechangia Tsh. 2,150,000/= za Maziwa na DC Waryuba ametoa Mifuko ya Sukari kwa Shule zote 43 za Wilaya ya Malinyi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.