Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba ameongoza Kikao cha Ushirika cha Tathmini ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani Wilaya ya Malinyi.Kikao hiko kimefanyika tarehe 23 Septemba 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
Mheshimiwa DC Waryuba amesema lengo la kuitisha Kikao ni kufanya tathmini kwa kujadili na kujua Ushirika Malinyi unaendaje mbele. Mheshimiwa DC Waryuba amesema kuna Miongozo inayoongoza kufanya mambo hayo ambayo ni Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 na Sheria ya Ushirika Namba 6 ya Mwaka 2013 zinaelekeza kutoa mafunzo kwa Vyama vya Ushirika ili kuhakikisha vyama vya Ushirika vinakuwa na uwezo wa kujisimamia hivyo Mheshimiwa DC Waryuba amesema hayuko tayari kuona Ushirika unadorora Malinyi kwani Watu wa kuutengeneza na kuusimamia Ushirika ni Wadau wa Ushirika wenyewe.
Katika Kikao hiko Mheshimiwa DC Waryuba ametoa maelekezo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa DC Waryuba anataka Msimamizi wa Maghala kwa Wilaya ya Malinyi awe mmoja kuanzia msimu wa zao la mbaazi.
Mheshimiwa DC Anataka Wataalamu wa Halmashauri waainishe Mbegu bora, Mbegu za aina gani zinatakiwa Malinyi.
Mheshimiwa DC ametaka Chama cha Ushirika UKIKU watoe Fedha kwa Vyama vya Msingi na Vyama vya Msingi ndivyo viwalipe Wakulima wao kuanzia msimu wa zao la mbaazi.
Mheshimiwa DC amezitaka AMCOS zote 22 zilizopo Malinyi ziajiri Makatibu, Wahasibu na Makarani.
Mheshimiwa DC amewataka UKIKU wafungue Ofisi yao Wilayani Malinyi ili wawe na mwakilishi atakayejibu hoja za Ushirika.
Mheshimiwa DC ameyataka Mabenki yaache Urasimu yawafuate Wakulima walipo
Mheshimiwa DC ametaka Wafanyakazi wa Mifugo waende kutoa chanjo za mifugo wenyewe, wasiwaachie wafugaji wachanje wenyewe.
Mheshimiwa DC ametaka kuwe na Orodha ya Wakulima (Data base) ili idadi ya wakulima ijulikane.
Mheshimiwa DC amewataka Chama cha Ushirika UKIKU waajiri wafanyakazi na wawape Mikataba ya Ajira.
Mwisho Mheshimiwa DC Waryuba amewaomba Wadau wa Ushirika ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 watumie haki yao wajitokeze kupiga Kura ya Rais, Mbunge na Madiwani.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.