Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba ameyasema hayo leo Novemba 23, 2024 wakati aliposhiriki Uchaguzi marathoni Wilayani Malinyi kwa lengo la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura Novemba 27, 2024.
DC Waryuba amesea kuwa huu ni wakati sahihi kwa Wananchi kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba kushiriki kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kipindi kingine cha miakaa itano.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Malinyi Ndugu Khamis Jaaphar Katimba amesema matarajio yake ni kuhakiksha kuwa asilimia 90 ya waliojiandikisha wanapiga kura.
Hata hivyo kwa Upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Malinyi Ndugu Abdulrahim Hamid amesema kuwa jukumu walilonalo Wananchi ifikapo tarehe 27 Novemba, ni kuhakikisha wanafanya maamuzi sahihi ya kuchagua chama kitakachopeleka mbele maendeleo ya Wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.