Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba mapema leo Oktoba 29,2025 asubuhi amepiga Kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Ngongwa.
Kwa upande wa Katibu Tawala Ndugu Saida Abbas Mhanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Katimba wao wamepiga Kura mapema asubuhi kwenye Kituo cha Lugala.
Hali ya Vituoni ni Shwari, Amani na Utulivu umetawala na unatoa fursa pana kwa Wananchi wa Wilaya ya Malinyi kujitokeza kupiga Kura na kutimiza wajibu wao wa kikatiba na kidemokrasia.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.