Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba amewaongoza Walimu wa Wilaya ya Malinyi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani. Maadhimisho hayo katika Wilaya ya Malinyi yameadhimishwa kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Nawigo, Kata ya Malinyi, Tarafa ya Malinyi tarehe 5 Oktoba 2025.
Maadhimisho hayo yamehusisha Michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza Kuku, Kuvuta Kamba, Mbio za Magunia,Kucheza Muziki, Mpira wa Pete (Netball), Modern Athletics na Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Mtimbira na Kombaini ya Malinyi na Ngoheranga ambapo kombaini ya Ngoheranga na Malinyi waliibuka na ushindi wa Penati 5-4.
Katika hotuba yake Mheshimiwa DC Waryuba alimshukuru Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumuachia kipande cha Ardhi cha Malinyi aendelee kukisimamia kama Mkuu wa Wilaya.
Mheshimiwa DC Waryuba aliongelea Falsafa ya "Mwalimu ni Ualimu na Ualimu ni Mwalimu" Mheshimiwa DC Waryuba amewataka Walimu wot, TSC,Mdhibiti ubora wa Elimu ya kuwa Siku ya Mwalimu ni Siku ya kutafakari na kuona walipotoka, walipo na wanapoelekea.
Mheshimiwa DC Waryuba amesema Mwalimu ni Ualimu na Ualimu ni Mwalimu maneno haya yana mantiki pana hakuna Mtu asiyekuwa zao la Mwalimu. Mheshimiwa DC Waryuba amesema zipo changamoto kwa Walimu zinatofautiana na yapo mambo makubwa Walimu wameyafanya.
Mheshimiwa DC Waryuba amewataka Walimu wajumuike na wenzao (Socialization) na kuwataka wasijidharau wala kujikinai.
Mheshimiwa DC Waryuba amesema Walimu ni Sayansi, Sanaa,Taaluma, Hakuna Nchi iliyoweza kuendelea bila Walimu. Pia ukitaka kocha mzuri wa mchezo wowote ule kama Riadha, Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete( Netball) utawapata kwenye Ualimu na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Khamis Katimba aangalie uwezekano wa kupeleka Timu ya Wachezaji wa Mpira wa Miguu kwenye Mashindano yajayo ya SHIMISEMITA.
Mwisho amewataka Walimu wajitokeze kupiga Kura ya Rais, Mbunge na Madiwani ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 na wahamasishe Amani na Utulivu uendelee katika Wilaya ya Malinyi kwani yapo Maisha baada ya Uchaguzi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.