Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba amewaongoza Wananchi wa Tarafa ya Ngoheranga kwenye Bonanza la kuhamasisha Maendeleo ambalo limefanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ngoheranga.
Bonanza hilo limehusisha Michezo mbalimbali kama Kukimbiza Kuku, Mashindano ya Kula, Maigizo, Mbio za Magunia, Sarakasi, Mpira wa Miguu Wanawake Tanga Princes vs Mabanda ambapo Tanga waliibuka kwa ushindi wa Penati 3=2. Upande wa Wanaume ilikuwa Sodo Master vs BICON ambapo BICON walishinda kwa Penati 5-4.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya katika Hotuba yake alitoa Shukrani kwa Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan. Amesema Daktari Samia amefanya mambo makubwa Malinyi kwenye Miundombinu, Elimu, Afya, Kilimo,Mifugo nk na hivi karibuni wakazi wa Ngoheranga wamepata Mahakama ya Mwanzo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema lengo la Bonanza ni kuhamasisha maendeleo na maendeleo yanaletwa na Watu. DC Waryuba amewahimiza Wananchi waendelee kuendeleza Maendeleo kwenye Sekta ya Kilimo, Uvuvi na Michezo. Amesema Wilaya ya Malinyi kuna haja ya kuwa na timu kubwa ya mpira wa miguu itakayoshiriki mashindano makubwa.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema lengo la Bonanza ni kuhamasisha maendeleo na maendeleo yanaletwa na Watu. Dc Waryuba amewahimiza Wananchi waendelee kuendeleza maendeleo kwenye Sekta ya Kilimo, Uvuvi na Michezo. Amesema Wilaya ya Malinyi kuna haja ya kuwa na timu kubwa ya Mpira wa Miguu itakayoshiriki mashindano makubwa.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewahamasisha Wafugaji wachanje Mifugo yao na Mifugo ipate hereni. Mheshimiwa DC Waryuba ametoa maelekezo kwa TAWA wakishirikiana na Afisa Wanyamapori waweke mikakati ya kuzuia Wanyama Pori waletao kero kwa Wananchi mfano Tembo.
Mheshimiwa DC Waryuba alielezea dhana ya Maendeleo ili Jamii iendelee inahitaji Watu,Ardhi,Uongozi Bora na Siasa safi. Mwisho amewaomba Wananchi wa Malinyi ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025. Wananchi wanatakiwa watimize haki yao kwa kujitokeza kupiga Kura ya Rais, Mbunge na Madiwani.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.