Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amewataka Wahitimu wa kozi ya jeshi la akiba kundi la 9 kwa mwaka 2024 kuzingatia nidhamu na kuwa mfano bora kwa jamii.
Dc Waryuba amesema hayo mwishoni mwa juma lililopita wakati akifunga kozi ya Jeshi la akiba kundi la 9 kwa mwaka katika Kata ya Biro.
DC Waryuba ameeleza kuwa pamoja na changamoto ya Wazazi /Walezi wa Kata hiyo kuwa na mwamko mdogo wa kuwaruhusu Vijana kushirki mafunzo hayo lakini Vjana 67 waliohitmu kozi hiyo wamefikia viwango vinavyokubalika kwa Askari wa Jeshi la akiba.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi ya kuhitimisha kozi ya Jeshi la akiba Diwani wa Kata ya Boro Mhe. Ernest Ndagwe amewaomba Wazazi/ Walezi kuwaruhusu vijana wao kushiriki program mbalimbali zinazotolewa na Serikali pindi fursa hizo zinapotokea kwaajili ya manufaa ya Taifa letu.
Aidha, Mhe, Ndagwe ameuomba Mhe. DC Waryuba kuwaangalia vijana hao kwa jicho la kipekee pindi zinapotokea fursa zinazoendana na mafunzo waliyopata katika kozi hiyo.
Sambamba na hilo Diwani Ndagwe amewakumbusha Wakazi wa Kata ya Biro kushiriki kikamilifu katika kuchagua Viongozi watakaowaongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano siku ya tarehe 27 ambayo ni siku maalum ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Hata hivyo, Taarifa ya awali imeeleza kuwa kozi hiyo imetolewa kwa kipindi cha wiki 18 mfulululizo huku ikitaja idadi ya wanafunzi 67 ambao wamehitimu kozi hiyo na kuongeza kuwa Wanafunzi 20 hawakufanikiwa kufika mwisho wa kozi hiyo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utoro, nidhamu, ugonjwa na wengine kutokufikia kiwango kinachokubalika
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.