Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Katimba amefungua Semina Elekezi kwa Viongozi wa Jamii na Watoa Huduma ya Afya ya Msingi kuhusu Saratani ya Matiti. Semina hiyo Elekezi kuhusu Saratani ya Matiti ambayo imefadhiliwa na Shirika la Jhpiego imefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Malinyi tarehe 2 Oktoba 2025.
Kwa upande wa mtoa Mada Daktari Emmanuel Chogo ambaye ni Daktari Bingwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Malinyi alielezea Saratani ya Matiti ni Ugonjwa unaotokana na chembe chembe hai katika Matiti ambazo hukua na kugawanyika bila udhibiti maalumu. Chembechembe hizo za Saratani zinaweza kusambaa kutoka kwenye matiti hadi sehemu nyingine za mwili kwa kupitia mfumo wa damu.
Dk.Chogo amesema ni muhimu kwa Wanawake na Wanaume kufahamu dalili za Saratani ya Matiti ili kuweza kuchunguza, kubaini na kupata tiba ya Saratani hiyo mapema. Daktari Chogo alielezea mambo mengi kwa mfano Jinsi ya kujilinda na Saratani ya Matiti, Tiba ya Saratani ya Matiti, Jinsi ya Kujikinga, Wajibu wa Viongozi wa Jamii kuhusiana na Saratani ya Matiti.
Kwa Upande wa DED Katimba aligusia kuhusu Mtindo Bora wa Maisha ili kulinda Afya ya Wafanyakazi, alisisitiza Suala la Lishe kwa Watumishi wa Umma na amewaomba wawe wanahudhuria mazoezi. Amesema " Afya is the First Capital" kila kitu tunacho " enjoy" na kufurahia ni kwa sababu ya Afya bora inabidi Watu wajiangalie kwenye Lishe na Afya.
DED Katimba amesema ili Ujumbe uwafikie Watu wengi zaidi amewaalika watoa Mada washiriki kwenye Kikao cha Halmashauri cha Tathmini ya Robo ya kwanza ya Mwaka kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 kitachofanyika tarehe 4 Oktoba 2025 kwenye Ukumbi wa Halmashauri.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.