Mapema leo tarehe 11 Oktoba, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amefanya uzinduzi rasmi wa zoezi la uandikishaji orodha ya Wapiga kura Katika Wilaya ya Malinyi.
Mhe. Waryuba ametekeleza zoezi hilo Kijijini kwake Misegese Kitongoji cha Salatogwa Kata ya Malinyi, Tarafa ya Malinyi Wiyani Malinyi.
Mara baada ya kujiandikisha Wakili Msomi Sebastian Waryuba alipata wasaa wa kuzungumza na Wakazi wa Kijiji cha Misegese waliokuwa wamekusanyika katika kituo hiko kwaajili ya kujiandikisha na kuwaomba Wakazi hao wawahamasishe wenzao ambao bado hawajajiandikisha waweze kujiandikisha ili waweze kuchagua Viongozi watakaowaongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano
Sambamba na hilo Mhe. Waryuba akishirikiana na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Jaaphar Katimba walitoa elimu ya kujiandikisha katika orodha ya Wapiga kura pamoja na elimu ya kupiga kura kwa Wakazi hao.
Aidha Mhe, Waryuba na Ndugu Khamis Jaaphar Katimba walijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Wakazi wa Kijiji cha Misegese kuhusu kujiandikisha katika orodha ya Wapiga kura pamoja na kupiga kura.
MALINYI TUMEAMUA, TUMEZINDUA NA TUNAENDELEA
"SERIKALI ZA MITAA, SAUTI YA WANANCHI, JITOKEXE KUSHIRIKI UCHAGUZI"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.