Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Katimba amefunga Mafunzo ya Mfumo wa FFARS katika tarafa ya Ngoheranga tarehe 18 Septemba 2025.Lengo la mafunzo hayo ni kutoa ujuzi dhidi ya mfumo wa matumizi ya Fedha za Serikali kwenye vituo vya kutolea huduma. Mafunzo hayo ya siku 2 kwa Wilaya ya Malinyi yamefanyika katika tarafa ya Mtimbira ambako kulikuwa na Washiriki 94, Malinyi washiriki 70 na Ngoheranga washiriki 50.Jumla Kuu washiriki 214.
Mafunzo hayo yaliwahusisha Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wanaofanya kazi za Kihasibu, Watendaji wa Kata na Vijiji, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Waganga Wafawidhi wa Zahanati na Vituo vya Afya.
Mkurugenzi Mtendaji alisisitiza kila Fedha inayokusanywa lazima ionekane kwenye Mfumo alishauri Washiriki watumie siku ya Jumatatu kuandaa Ripoti na Jumanne kuangalia ripoti na kujadili. DED Katimba alisisitiza Vijiji wasimamie mapato ya makusanyo ya Vijiji na kila Kata Wajumbe wa Menejimenti ya Kata( Ward Management Team) Kila Mjumbe awe mlezi wa Kijiji ili aweze kujua mambo "technical issues" ndani ya Kijiji kwa uzuri na ufasaha zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji aliwahimiza Washiriki kuendelea kuhamasisha kusimamia miradi na kufatilia biashara zipi zina vibali halali/leseni za biashara.
DED Katimba amesema Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi imepokea Fedha Taslimu Tsh. Billioni 1.5 toka Serikali Kuu na mapato ya ndani kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.