Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ys Malinyi Ndugu Khamis Katimba amefungua Kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Malinyi.Kikao hiko kimefanyika Makao Makuu ya Halmashauri tarehe 14 Julai 2025.
Katika Kikao hicho DED Katimba alipata nafasi ya kuwafahamu Watumishi Wapya, Katika Kikao hiko DED Katimba aliwaelekeza ya kuwa sekta ya Maendeleo ya Jamii ni kubwa na pana sio kuangalia Mikopo tu ya asilimia kumi (10%)
Maafisa Maendeleo ya Jamii ni Makatibu na Waratibu wa Shughuli za Kata hivyo ni lazima wajue Ishu(Issues) zote zinazoihusu jamii, Kila kitu chenye manufaa ya Jamii Afisa Maendeleo ya Jamii anatakiwa ajue.
Amewataka wawe na taarifa ya vyanzo vya Mapato. Wanatakiwa wapate muda wa kwenda kuangalia vyanzo na waweke ratiba ya kutembelea Kata. Kata nzima iwe kichwani mwa Afisa Maendeleo ya Jamii. Amewataka wawe active muda wote wanatakiwa wajue mambo mengi hawana mipaka ya kutokujua mambo.
Katika Kikao hiko Mada mbalimbali ziliwasilishwa kwa Washiriki kama vile TASAF, ICHF, HIV/AIDS, Lishe,Mazingira, Nyumba Bora na Ukusanyaji Takwimu.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.