Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Katimba ameyasema hayo mapema leo Juni 5, 2025 wakati akufungua mafunzo ya ufahamu kuhusu Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TADB kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wa Malinyi Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo Misegese Yalilenga kuwajengea uwezo Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kutambua fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo.
Katimba amesemba kuwa Mkoa wa Morogoro una mazao matano ya kimkakati ambayo Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Kighoma Malima anayasimamia ikiwa ni pamoja na chikichi, parachichi, kokoa, karafuu na korosho, hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo ya TADB kutumia fursa hizo ili kufikia malengo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.