Halmashauri za Mkoa wa Mororogoro hususan sekta ya mapato zimetakiwa kuiga mfano wa Afisa mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi Agness Lyanga ambaye ameibuka Mwanamke kinara katika Mkoa wa Morogoro kwa ukusanyaji na usimamizi mzuri wa mapato kwa asilimia 98 kwa kipindi cha mmiezi 8.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya wakati akimkabidhi Bi Agness Lyanga zawadi ya fedha taslim sh 500,000 katika maadhimisho ya siku ya Wanawake yaliyofanyika K8mkoa Machi 8, 2025 katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
“Agness Lyanga ni Mwanamke pekee na kinara katika Mkoa wa Morogoro aliyeiwezesha Halmashauri yake kukusanya mapato kwa asilimia 98 kwa kipndi cha miezi 8,Halmashauri zingine Mkoani Morogoro igeni mfano kwa Mwanamke huyu kinara kutoka Malinyi” amesema DC Kyobya.
Kwa upande wake Mkuugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Jaaphar Katimba amesema kuwa Wajumbe wa Kamati tendaji ya Halmashauri (CMT) katika kikao cha mwezi februari walipendekeza kuwa Bi Agness Lyanga apewe zawadi ya shilingi 500,000 ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kutambua jitihada zake katika sekta hiyo ya mapato kwa kipindi cha mwaka 2024/2025 ambapo pendekezo hilo lilikubaliwa na Wajumbe wote wa Kamati tendaji ya Halmashauri na kukubaliana kumkabidhi zawadi hiyo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake.
Naye Mwanamke Kinara Mkoani Morogoro kwa mwaka 2025 Agness Lyanga amesema kuwa amefarijika sana kuona kwamba jitihada zake zimetambuliwa na kuthaminiwa, na kuongeza kuwa zawadi hiyo imempa hamasa ya kuendelea kujituma na kufanya vizuri Zaidi.
"Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe haki usawa na uwezeshaji"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.